Latest Updates

Breaking News....HUKUMU YA YONA, MRAMBA NA MGONJA YAPIGWA TAREHE HADI JULAI 6

Gray Mgonja (mbele) akiwa na Basil Mramba (wa pili kushoto) wakiwa eneo la mahakama. (Picha na Maktaba Yetu)
HUKUMU ya aliyekuwa Waziri wa Fedha, Basil Mramba, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Gray Mgonja na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Daniel Yona, imeahirishwa tena katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo hadi Jumatatu ya Julai 6, mwaka huu saa 7 mchana.
Kesi hiyo imeahirishwa baada ya mmoja wa jopo la mahakimu wanaosikiliza kesi hiyo kuwa mgonjwa na kwa ushauri wa daktari ni kwamba anahitaji mapumziko. Hivyo hukumu hiyo itasomwa Jumatatu ijayo.
Watuhumiwa hao wanakabiliwa na mashtaka ya matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia serikali hasara ya Shilingi bilioni 11.7.

0 Response to "Breaking News....HUKUMU YA YONA, MRAMBA NA MGONJA YAPIGWA TAREHE HADI JULAI 6"

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...