Jeshi
la Uganda linasema kuwa kiongozi wa kundi la waasi linalolaumiwa kwa
mauaji ya karibu watu 1000 amekabidhibiwa Uganda baada ya kusafirishwa
kutoka nchini Tanzania.
Jamil Mukulu ambaye alikamatwa nchini
Tanzania mwezi Aprili, ni kiongozi wa kundi la ADF ambalo limelaumiwa
kwa kuendesha mashambulizi mashariki mwa Uganda na mji mkuu Kampala.Pia anatakikana kwa mashtaka yanayohusiana na vita nchini Jamhuri ya Demokrasi ya Congo.
Jeshi la Congo liliendesha oparesheni kubwa dhidi ya waasi wa ADF mwaka uliopita.


0 Response to "Kiongozi wa ADF akabidhiwa Uganda"
Post a Comment