
Maofisa wa usalama barabarani wakichukua taarifa eneo la ajali.
Coaster baada ya kuigonga treni.
Wananchi wakishuhudia ajali hiyo.
WATU
watano wamepoteza maisha huku 24 wakijeruhiwa baada ya basi la abiria
kuligonga treni lililokuwa linatoka Morogoro – Dodoma leo Jumatano
asubuhi katika eneo la Kibaoni, wilayani Kilosa mkoani Morogoro. Basi lililohusika katika ajali hiyo ni aina ya Isuzu Coaster lenye namba za usajili T837 CTM linalomilikiwa na Feisal A. Khuwel wa wilayani Kilosa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kueleza kuwa ajali hiyo imetokea leo (Jumatano) majira ya saa 1 asubuhi na imetokana na uzembe wa dereva wa basi.
Naye Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wiaya Kilosa, Dickson Masale amethibitisha kupokea miili ya watu watano akiwemo dereva wa basi pamoja na majeruhi 24.




0 Response to "MAJONZI HAYA!!!!:HIVI NDIVYO WATU WALIVYOPOTEZA MAISHA BAADA YA KUGONGWA NA TRENI!!!"
Post a Comment