Taarifa ninayokusogezea ni hii kuhusu kituo cha polisi eneo la ‘Bunju A’ Dar es Salaam kilichochomwa moto na wananchi baada ya tukio la ajali ya gari kumgonga mtoto mmoja.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, Camillus Wambura
‘Hapa kituo kimechomwa moto lakini kabla ya uchomwaji wa kituo hiki
kulikuwa majira ya asubuhi kati ya saa moja na nusu kulikuwa na tukio la
ajali lililosababisha kifo hapa maeneo ya Bunju A majira hayo gari moja
aina ya Coast ilikuwa ikitoka Bagamoyo na kusababisha kumgonga
mwanafunzi Thabisa Omary mwenye umri wa miaka 11 anasoma Bunju A darasa
la nne n ilisababisha kifo chache’ – Camillius Wambura (RPC)
‘Kwahiyo kutokea kwa ajili hiyo
wanafunzi waliweza kuingia Barabara wakaziba barabara zote kuanzia Bunju
A mpaka Bunju B wakilalamika kwamba awali kulikuwa na Matuta lakini
matuta na sasa magari yanapita kwa mwendo kasi na kusababisha vifo
lakini walitoa matamko kwamba wanataka watu wenye mamlaka na Barabara
wafike na kuweka matuta kama yalivyokuwa ili yaweze kupunguza Ajali na
vifo’ – Camillius Wambura (RPC)
‘Sasa baada ya sisi Polisi kufika na
kusikia tamko hilo tuliwasiliana na mamlaka ya Tan Road walituma watu
kuja kuwasikiliza wanafunzi wale lakini kuona maeneo ambayo
yanalalamikiwa kwamba yalikuwa na matuta na hayana basi nakujua ni hatua
gani wanaichukua kuweza kwanza kuendana na malalamiko hayo lakini pia
kupunguza ajali kama inavyodaiwa’ – Camillius Wambura (RPC)
‘Ilikuwa ni bahati mbaya sana wakati hao
Tanroad wamefika na wakati wanaanza survey ya maeneo hayo kulitokea
uhamasishaji ambao hakuwa wa lazima hakuwa wa maana kwasababu suala
lilikuwa ni wa matuta uhamasishaji huo ulisababisha vurugu na kuanzia
kurusha mwe na kundi kubwa lilitoka katika pande mbili za barabara
kuanza kurusha mawe’- Camillius Wambura (RPC)
‘Jeshi la polisi kwa askari waliokuwepo
walijaribu kuwatawala wale watu hayo pasipo kuleta madhara kwasababu
tunajitahidi kupunguza madhara kwa kilengo cha hali ya juu kwa hiyob
waliwatala pasipo kuleta madhara lakini kundi hilo hilo lilikuwa kubwa
wakaweza kukivunja kituo kidogo cha polisi kilichopo hapa Bunju A na
kukiteketeza kwa moto hapa ndani kulikuwa na maabusu watatu ambao
ilibidi askari wawafungulie na kuwaamisha ili kuokoa maisha yao’-
Camillius Wambura (RPC)
‘Kwa hiyo waliofanya kitendo hiki
hatutawacha waendele kuchoma vituo vingine na nyumbani nyingine
tutahakikisha tunawakamata wote kila mmoja na tutahakikisha
tunawafikisha mbele ya vyombo vya dola mchezo huu ni uhuni lakini mchezo
huu ni uhalifu hiki ni kituo kilichojengwa na wananchi wenyewe ni kituo
kilichokuwa kinawahudumia wao wenyewe’ – Camillius Wambura (RPC)






















0 Response to "Picha 11 za kituo cha Polisi kilichochomwa moto leo Dar"
Post a Comment