Na Gladness Mallya
BAADA ya
hivi karibuni kutangaza nia ya kugombea ubunge wa Viti Maalum kwa tiketi
ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) huko Morogoro Vijijini alikozaliwa, staa
wa sinema za Kibongo, Wastara Juma ameibuka na kueleza kwamba ameamua
kufanya hivyo ili kuwatetea walemavu na watoto wa kike.
Akipiga stori na Ijumaa, Wastara alisema wananchi ambao ni walemavu
wamekuwa hawatendewi haki katika maeneo mbalimbali kulingana na maumbile
yao hivyo lengo lake kubwa ni kwenda kutetea haki zao ili ziwe sawa na
watu wengine pamoja na sanaa kwani wasanii wamekuwa wakinyonywa kutokana
na kazi zao kuuzwa hovyo.
Naamini nitashinda, kwani jimbo nililochagua mimi ni mzaliwa na
nimekuwa mwakilishi wa akina mama na watoto kwa muda mrefu. Sasa ni
wakati wa kwenda kuwawakilisha huko bungeni, alisema Wastara.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



0 Response to "WASTARA ATAJA SABABU ZA KUGOMBEA UBUNGE"
Post a Comment