Home » MATUKIO
Showing posts with label MATUKIO. Show all posts
Showing posts with label MATUKIO. Show all posts
HATARI: KITUO CHA POLISI DAR CHAVAMIWA NA MAJAMBAZI DAMU YAMWAGIKA, YAANI NI DAMU KILA SEHEMU
Posted by Unknown
at 8:49 AM,
Add Comment
Read more
VIDEO.....HAYA NDIO MANENO YA MNYIKA KUMTAMTAKA SPIKA KUSITISHA SHUGHULI ZA BUNGE LEO
Posted by Unknown
at 4:46 PM,
Add Comment
Read more
MAAJABU HAYA!!!!....Tohara ya Milimani Afrika Kusini


Mrengo wa vijana katika chama tawala Afrika Kusini{ANC Youth League} umesema unapanga kufanya sherehe ya tohara ya kitamaduni kwenye milima maalum.
Shirika la Turathi la Umoja wa Mataifa{UNESCO} limetangaza eneo hilo la "Table Mountains" kuwa turathi kwa sababu kuna mimea ya kipekee. Kuna aina elfu tano ya mimea kwenye milima hiyo.

Taarifa ya vijana hao wa ANC jimbo la Western Cape imesema hakuna arthi ya kufanyiwa tohara ya utamaduni. Haijabainika ikiwa watapata idhini kuendesha shughuli hiyo
Posted by Unknown
at 4:29 PM,
Add Comment
Read more
Breaking News....HUKUMU YA YONA, MRAMBA NA MGONJA YAPIGWA TAREHE HADI JULAI 6
Gray Mgonja (mbele) akiwa na Basil Mramba (wa pili kushoto) wakiwa eneo la mahakama. (Picha na Maktaba Yetu)
HUKUMU ya aliyekuwa Waziri wa Fedha, Basil Mramba, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Gray Mgonja na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Daniel Yona, imeahirishwa tena katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo hadi Jumatatu ya Julai 6, mwaka huu saa 7 mchana.
Kesi hiyo imeahirishwa baada ya mmoja wa jopo la mahakimu wanaosikiliza kesi hiyo kuwa mgonjwa na kwa ushauri wa daktari ni kwamba anahitaji mapumziko. Hivyo hukumu hiyo itasomwa Jumatatu ijayo.
Watuhumiwa hao wanakabiliwa na mashtaka ya matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia serikali hasara ya Shilingi bilioni 11.7.
Posted by Unknown
at 1:39 PM,
Add Comment
Read more
BREAKING NEWS.....BUNGE LAAHIRISHWA TENA


SPIKA wa Bunge, Anne Makinda ameahirisha bunge baada ya kutokea mzozo kwa wabunge wa upinzani kusimama na kuomba mwongozo wakati Waziri wa Nishati na madini, George Simbachawene alipoanza kusoma kwa mara ya pili Muswada juu ya Petroli, 2015 (The Petroleum Act, 2015).
Baadhi ya wabunge wa upinzani walisimama kuomba mwongozo akiwemo, Tundu Lissu lakini hawakupewa nafasi ndipo wenzao nao waliposimama na kuanza kupaza asauti wakiomba mwongozo.
Spika aliahirisha bunge hilo huku akiwataja kwa majina baadhi ya wabunge wanaodaiwa kuanzisha fujo bungeni
Posted by Unknown
at 12:45 PM,
Add Comment
Read more
NYOKA AZUA KIZAAZAA MORO LEO....WAAMKA KULA DAKU, WAMKUTA NYOKA MWENYE HIRIZI!

Dustan Shekidele, Morogoro
Inatisha! Ndani ya Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, familia ya mwanaume aliyetambuliwa kwa jina la Hamis Juma, imekumbwa na mauzauza baada ya kuamka ili kula daku na kukutana na nyoka mwenye hirizi mlangoni.
Tukio hilo lililozua taharuki lilijiri mapema wiki hii kwenye nyumba ya familia hiyo inayoishi Mtaa wa Mkota Kata ya Kiwanja cha Ndege mjini hapa.
Baada ya kutonywa juu ya tukio hilo, Ijumaa lilifika kwenye familia hiyo alfajiri na kushuhudia nyoka huyo aliyekuwa na hirizi na kitambaa cheusi shingoni akiwa mlangoni.
Akisimulia kisa hicho baba wa familia hiyo, Hamis alisema kuwa waliamka saa 7:00 usiku ili kupata daku kama kawaida kwani walianza kufanya hivyo tangu walipofunga.
“Wakati tukiwa sebuleni tunakula, tulianza kuona damu nzito ikisambaa kutokea mlangoni.
“Ukweli tulishtuka sana. Tulipofungua mlango tulishtuka kuona nyoka mkubwa mlangoni akiwa na hirizi huku damu zikiendelea kusambaa kutoka pale alipokuwa yule nyoka.
“Ilibidi tufunge mlango hadi alfajiri tuliamua kuwaita watu waje kushuhudia na kusaidia kumuondoa,” alisema Hamis.
Katika kutafuta msaada wa kumuondoa nyoka huyo na kusafisha damu zilizozagaa, alitokea mjomba wa familia hiyo ambaye jina halikupatikana akaanza kumtoa kwa kutumia mti, jambo lililosababisha taharuki kwa watu waliokuwepo wakaanza kukimbia.
Baada ya kumtoa nyoka huyo, watu walianza kumpiga wakitaka kumchoma moto lakini alitokea mwanaume asiyefahamika akamkwapua na kuanza kukimbia naye mitaani.
Katika hali ya kushtua zaidi, nyoka huyo alibadilika, akawa hana hirizi huku akionekana ‘kadogo’ jambo lililoibua madai ya ushirikina hivyo watu wakamuua.
Baba mwenye nyumba hiyo, Hamis Juma.
Kwa upande wake mke wa Hamis, Mama Nurdin ambaye ni mjumbe wa mtaa huo, alishtushwa na tukio hilo na kusema familia yake imekumbwa na hofu kubwa.
Uongozi wa Kata ya Kiwanja cha Ndege ukiongozwa na Diwani, Mohamed Matikula na Afisia Mtendaji, Diha Zongo walifika eneo la tukio na kuwachukua baba na mama wa familia hiyo hadi ofisi ya kata kwa mahojiano zaidi.
Posted by Unknown
at 10:24 AM,
Add Comment
Read more
Boko Haram Yashambulia Zaidi 150Wapoteza Maisha


Watu 150 wameuawa baada ya Boko Haram kuvamia kaskazini mashariki mwa Nigeria.
Walioshuhudia
mashambulizi hayo wanasema watu tisini na saba wameuawa siku ya
Jumatano katika kijiji cha Kukawa kilichopo karibu na Ziwa Chad.Habari zinasema pia wanaume 48 wamepigwa risasi na wapiganaji katika mashambulizi tofauti siku ya Jumanne.
Mashuhuda wanaokimbia eneo lililopo karibu na Ziwa Chad wanasema idadi kubwa ya wapiganaji wamevamia vijiji vitatu ambapo wameuwa wanaume, wanawake na watoto.
Baadhi ya ripoti zinasema walipigwa risasi huku wengine wakielezea jinsi wapiganaji hao walivyowachinja watu na kuchoma majengo.
Upande wa Kusini, nje kidogo na mji wa Monguno, kundi la wapiganaji wa Boko Haram wamefika usiku wakati watu walipokuwa wanaswali. Waliwasubiri mpaka walipomaliza kuswali na kuwatenganisha wanaume na wanawake na baadae kuanza kuwamiminia risasi wanaume.
Mwanasiasa anayewakilisha eneo hilo, Mohammed Tahir amesema awali alitoa tahadhari kwa jeshi la Nigeria kwamba vijiji hivyo viko hatarini kwa sababu Boko Haram wameweka makazi katika maeneo hayo baada ya kutimuliwa katika himaya yao ya msitu wa Sambisa.
Haya ni mashambulizi mabaya zaidi kufanywa na Boko Haram katika kipindi cha wiki kadhaa.
Kundi hilo limekuwa likilipuwa mabomu kadhaa baada ya kudhoofishwa na majeshi ya Nigeria.
Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari amesema kipaumbele chake ni kuimarisha mapambano dhidi ya Boko Haram.
Posted by Unknown
at 9:19 AM,
Add Comment
Read more
PICHAZ....HIZI NDIZO AJALI MBAYA ZILIZOVUNJA REKODI TANZANIA
Posted by Unknown
at 11:39 AM,
Add Comment
Read more
Subscribe to:
Posts (Atom)















