Dar es Salaam.
Kauli ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye bado inawaumiza vichwa wapinzani nchini baada ya viongozi hao jana kuitamkia wazi Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), kuwa hakuna haja ya kujadili maadili wakati CCM tayari kimesema ‘kitafunga bao la mkono.’
Wakizungumza kwenye mkutano kati ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na viongozi wa vyama vya siasa kuhusu maadili ya Uchaguzi jana, baadhi ya viongozi hao walitaka mkutano huo usitishwe hadi pale CCM itakapomuonya Nape.
Wa kwanza kuibua mada kuhusu Nape, ni Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha NLD, Dk Emmanuel Makaidi ambaye alisema hakuna haja ya kuendelea na mkutano huo hadi NEC, Msajili wa Vyama vya Siasa na IGP wakemee kauli hiyo.

“Hivi tutayazungumziaje maadili, mbona CCM kimeshaonyesha kuwa
hakitafuata maadili, kuna haja gani ya kuzungumzia wakati wameshasema
watafunga hata kwa goli la mkono?” alisema Dk Makaidi.
Awali akiwa katika ziara ya Kinana wilayani ya Sengerema, Nape
alikaririwa akisema kuwa ana uhakika CCM itashinda baada ya kuona
mwitikio mkubwa wa Watanzania katika ziara hizo.
“Rangi inayoenda Ikulu ni hii (anaonyesha shati lake la kijani
ambayo hutumiwa na chama hicho). Tuna uhakika na ushindi wa Rais. Kwa
namna yoyote ile, CCM itarudi Ikulu hata kama ni kwa bao la mkono... bao
ni bao tu ili mradi refa hajaona,” alisema Nape.
Hata hivyo, Mwenyekiti wa NEC, Jaji Damian Lubuva aliwatoa
wasiwasi wanasiasa hao akiwaambia kuwa Nec itafanya uchaguzi kwa
kuzingatia sheria, kanuni na taratibu na hivyo kauli ya Nape haiwahusu.
“Maadili tunayoyatengeneza yataanza kutumika kuanzia Agosti 22,
wakati wa kampeni, lakini iwapo kuna vurugu zinatokea baina ya vyama
sisi wala Nec hatuhusiki,” alisema.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Wilbroad Slaa
akichangia kipengele cha wahusika wa maadili aliitaka Nec kuliweka Jeshi
la Polisi kupitia IGP kusaini na kuwa mhusika katika masuala ya maadili
ya uchaguzi.
Hiki kipengele cha 1.3 kinawataja wahusika wa maadili kuwa ni
vyama vya siasa, wagombea, Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Nec pekee.
“Kutokana na uzoefu tulionao katka chaguzi zilizopita, Jeshi la
polisi ni washiriki wakubwa katika masuala ya uchaguzi, kama jeshi hilo
halitasaini maadili hayo basi kutakuwa na matatizo makubwa katika
uchaguzi huo,” alisema.
Awali akifungua mkutano huo Jaji Lubuva alivitaka vyama vya
siasa kufuata maadili, sheria na kanuni za uchaguzi, na katika kipindi
chote cha kuanza kwa kampeni hadi siku ya uchaguzi.
Alisema kila chama na mgombea kitatakiwa kuheshimu na kutekeleza
kanuni na sheria za uchaguzi, siku moja baada ya uteuzi wa mgombea ili
kuepesha vurugu zinazotokea kipindi cha uchaguzi.
“Maadili tutakayojadili leo (jana), yatahusisha mambo mbalimbali
yasiyotakiwa kufanywa na vyama vya siasa na wagombea wao kipindi cha
kampeni hadi uchaguzi,” alisema Jaji Lubuva na kuongeza kuwa;
“Mfano kwa vurugu za aina yoyote katika mkutano wa chama kingine
cha saiasa, sanjari na maadili yanatakiwa kufuatwa wakati wa upigaji
kura hadi kutangazwa kwa matokeo.
(CHANZO: MWANANCHI)
(CHANZO: MWANANCHI)

0 Response to "KIZAAZAA....‘BAO LA MKONO’ LA NAPE LATUA TUME YA UCHAGUZI"
Post a Comment