Mwenyekiti wa Baraza la Wazee
la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Hashim Juma Issa
(kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam
jana mchana, kuhusu kongamano litakalo wakutanisha wazee wote bila
kujali itikadi za vyama vyao litakalo jadili mustakabali wa taifa
kuelekea uchaguzi mkuu litakalofanyika leo ukumbi wa Hoteli ya Blue
Pearl Ubungo jijini Dar es Salaam.
Makamu Mwenyekiti wa Baraza
la Wazee la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Suzan Lymo,
akizungumza katika mkutano huo.
Baadhi ya wazee wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mkoa wa Dar es Salaam wakiwa kwenye mkutano huo.
Baadhi ya wazee wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mkoa wa Dar es Salaam wakiwa kwenye mkutano huo.
Na Dotto Mwaibale
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema), kimeandaa kongamano la wazee ambalo litafanyika Hoteli ya
Blue Pearl jijini Dar es Salaam leoo.
Akizungumza katika mkutano na waandishi
wa habari jana mchana Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la chama hicho,
Hashim Juma Issa alisema kongamano hilo litawahusisha wazee wote nchini
bila ya kujali itikadi za vyama vyao.
Alisema dhima kubwa ya kuanzisha
kongamano hilo ni kuwapa elimu wazee bila kujali itikadi zao za kisiasa
hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu.
"Wazee wengi wamekuwa hawafahamu nini
majukumu yao kama wazee lakini kongamano hili litakuwa ndiyo chanzo
kikubwa cha kuwafahamisha wazee majukumu yao hasa katika wakati huu wa
kuelekea uchaguzi," alisema Issa.
Alisema kila mtu anafahamu binadamu huwa
anapitia hatua muhimu za maisha nazo ni utoto,ujana na utu uzima hivyo
hamna budi wazee hawa kuelewa lengo kuu katika katika uchaguzi mkuu huo
kuwa katika mstari ulinyooka.
"Kumekuwa na tabia ya Chama cha Mapinduzi
(CCM) kuwatumia wazee kwa ujanja tena hasa wakiwa na matatizo na
kuwabagua wa vyama vingine lakini sisi katika kongamano hili hatutobagua
mzee wa chama chochote katika kongamano hili kwani wazee wote ni
hazina,"alisema
"Hakuna asiyefahamu kuwa kwa sasa nchi
inaelekea katika uchaguzi mkuu ambao uchaguzi huu utakuwa ni mkubwa na
wa aina yake hivyo kwa kuwaita wazee hawa itakuwa ni muendelezo wa
kupata hekima zao kama wazee"alisema.
Issa alisema katika uchaguzi mku wazee
wana jukumu kubwa la kuhakikisha kushiriki kikamilfu katika zoezi zima
la kujiandikisha na kupiga kura ipasavyo.
Alisema hatua hiyo haina budi
kuwasahawisi watoto na watu wakubwa na wajukuu kushiriki kwa ukamailifu
katika tukio hili kwani kila mtu anahitaji mabadiliko katika nchi.
Hata hivyo Issa alisema wazee pia wana
jukumu kubwa la kutatua migogoro ,kushawisi na kusimamia maadili lengo
likiwa ni uthubutu wa kukemea viongozi wanaopata madaraka kwa njia ya
rushwa na ufisadi.
Alisema wanahitaji wazee watakaosimama kidete na kupaza sauti zao katika kukemea maovu na watenda maovu bila kuona haya.
Alisema katika kongamano hilo mgeni rasmi
anatarajiwa kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho Wilbroad Slaa huku mada
mbalimbali zitatolewa na Mabere Marando pamoja na viongozi wa dini ili
kuwapa elimu wazee kutokana na maadili ya nchi kumomonyoka kwa kiasi
kikubwa.


0 Response to "CHADEMA KUFANYA KONGAMANO BABU KUBWA LA WAZEE DAR"
Post a Comment